Mimi ni mhandisi wa mambo ya mionzi ya mawasiliano ya radio,lakini muda ambao sina kitu cha kufanya napenda sana kusoma hadithi za maisha ya watu mbali mbali waliofanikiwa katika sehemu mbalimbali za fani zao kwa juhudi,maarifa na jasho lao wenyewe.Hadithi hizi zinasisimua ndoto kwangu na kwa watu wengine kufanya mambo makubwa yaliyomo kwenye ndoto.Napenda hasa watu hao wakiwa watanzania wenzangu.Hadithi za mafanikio ya watu.Kwa hivyo basi kama una hadithi yoyote ya mtu aliefanikiwa au kama wewe umefanikiwa na unataka niiandike hadithi yako basi nitumie email nami nitaipublish.