Sikiliza Clouds FM Live station ya watu.

Wednesday, March 31, 2010

Rapa mashuhuri Flesh-n-bone wa Bone thugz n Harmony akamatwa na polisi akipafomu on stage.


Jina lake kamili ni stanley Howse alikamatwa jana akiwa kwenye stage akipafomu na grupu lake mjini cleveland Ohio kwenye ukumbi wa house of blues usiku wa saa sita.Soo alilokamatwa nalo ni la mwaka 1998 alimpiga na kikumbo cha bastola mama yake mzazi,ambaye alikuwa anajaribu kumuamulia asigombane na mtu mwingine.Mama yake alijeruhiwa vibaya kichwani,na pia watu kadhaa walijeruhiwa.Polisi juzi walijitetea kwamba hawakuwa na nia ya kuharibu show ila baada ya mtu kumtonya Flesh N bone kwamba ndata zimemzunguka na kwamba wanamsubiri,jamaa akawaanataka kuporonyoka stejini na kutoka kutokea kwenye dirisha la chooni ndipo wakamdaka.
Moja kati ya nyimbo zao nilikuwa nazizimia ni ule wa "home" ambao walimshirikisha phil collins.Anyway natumaini atatoka na kuendelea kusambaza burudani kama kawaida.

Jamani mtamu wangu( mysweetie) umepata barua kutoka kwa nani tena mbona waniogepesha?

Michelle alipata barua akitembea nje kwenye bustani yake ya ikulu kutoka kwa mtoto mdogo.Alikuwa anamuuliza kama anapenda ice cream na cake,na kwamba angefurahi kama angetembelea shule yake.Halafu alimwandikia kwamba msalimie na Barack.Michelle akaamua amuite Barack aisome mwenyewe.Huko Afrika kwetu yaani Raisi asome barua kutoka kwa mtoto au akae  kujibu maswali ya watoto ni kitu hakionekanagi mara nyingi.Nakumbuka shule niliyosoma muhimbili pimary yaani mwalimu mkuu akitokea tu inabidi ukimbie manake anaweza akakuwasha viboko vitatu au vinne kwa kuzulula hovyo.Labda tutafika siku moja kujua kwamba binadamu wote ni sawa,na wanahaki ya kusikilizwa bila kujali umri wala kabila.

Jinogee wanajeshi wa rwanda wakicheza twisti baada ya ushindi wa vita.

Monday, March 29, 2010

President Kagame in London for The Commonwealth Flag raising Ceremony- London, 8-11 March 2010



              Wa kwanza Kushoto ni mke wa Nwanko Kanu,halafu wa pili kushoto hahitaji kutambulishwa kama wewe ni mshabiki mzuri wa mpira wa miguu au timu iliyokuwa ikiitwa super eagles,halafu mzee mzima Kagame na his beloved gorgeous wife Jeanette.
              Nchi ya Rwanda sasa imekuwa mwanachama kamili wa jumuiya ya madola.Hii ni muungano wa nchi zote zilizowahi kutawaliwa na Uingereza.Mojawapo ya faida za kujiunga huko ni makubaliano mazuri kati ya nchi wanachama ya kuuza na kununua bidhaa mbalimbali kwa masharti na gharama nafuu.Kazi nzuri Paul.