Sikiliza Clouds FM Live station ya watu.

Wednesday, March 31, 2010

Rapa mashuhuri Flesh-n-bone wa Bone thugz n Harmony akamatwa na polisi akipafomu on stage.


Jina lake kamili ni stanley Howse alikamatwa jana akiwa kwenye stage akipafomu na grupu lake mjini cleveland Ohio kwenye ukumbi wa house of blues usiku wa saa sita.Soo alilokamatwa nalo ni la mwaka 1998 alimpiga na kikumbo cha bastola mama yake mzazi,ambaye alikuwa anajaribu kumuamulia asigombane na mtu mwingine.Mama yake alijeruhiwa vibaya kichwani,na pia watu kadhaa walijeruhiwa.Polisi juzi walijitetea kwamba hawakuwa na nia ya kuharibu show ila baada ya mtu kumtonya Flesh N bone kwamba ndata zimemzunguka na kwamba wanamsubiri,jamaa akawaanataka kuporonyoka stejini na kutoka kutokea kwenye dirisha la chooni ndipo wakamdaka.
Moja kati ya nyimbo zao nilikuwa nazizimia ni ule wa "home" ambao walimshirikisha phil collins.Anyway natumaini atatoka na kuendelea kusambaza burudani kama kawaida.

1 comment:

  1. yaani atoke mtu aliye mjeruhi mama yake mzazi? r u kidding us? he belongs there, let him stay there forever

    ReplyDelete