Alizaliwa april 4th,1987 kamukunji Kenya.Anaongea kiswahili cha kuchekesha cha kikenya ambacho mara nyingi kimechanganyika na maneno ya kizungu na lafudhi za kikuyu.Sisi wa Tanzania tunakiita kiswanglish.Ameenda high school ya kamukunji na ni mtoto wa mkulima wa kawaida tu Kenya.Ni mchezaji wa mpira wa miguu na nafasi yake ni ulinzi wa kati (midfield). January 2010 Inter Milan ambayo ni klabu kubwa ya daraja la kwanza nchini itali ilimnunua kutoka Parma(klabu nyingine kubwa ya daraja la kwanza) ilimnunua kwa yuro million mbili sawa na dola million nne za kimarekani,manake club yao inahitaji mlinzi wa kati vibaya sana na Micdonald ndio mwenyewe haswa.Amesaini mkataba wa miaka minne.Mmoja kati ya mashabiki wake wakubwa ni waziri mkuu wa kenya Raila Odinga ambaye alitumia masaa matatu ya simu kutoka afrika akiongea na Gordon brown ili Mcdonald apewe kibali cha kufanya kazi ndipo aweze kuichezea Manchester City ambayo ni timu kubwa na ya daraja la kwanza Uingereza.Manchester City walikuwa wa kwanza kumng'angania na walikuwa tayari kumpa dau kubwa lakini sheria ngunguri na za kibaguzi za kiingereza zilimzuia.Mungu ambariki katika safari yake hiyo labda siku moja ataweza kufungua milango kwa waswahili wengine pia.Juhudi na kipaji cha mtu kinaweza kumfikisha mtu na hata kuinua jamii yake hadi juu kabisa.
Wednesday, February 17, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment