Alexander haig,jr alianza career yake kama mwanajeshi wa kawaida wa jeshi la Marekani mwaka 1947.Aliendelea kupanda cheo Jeshini Mpaka akafikia cheo cha Vice chief of staff of the Army.kwa kifupi ni bosi namba mbili wa jeshi la marekani(number two ranking-officer in the army).
Baada ya mafanikio makubwa jeshini Raisi Richard Nixon akamchagua kama msaidizi wake katika ushauri wa mambo yanayohusu usalama.Na mwaka 1981 mwezi wa kwanza raisi Regan aliona Haig anamsaada mkubwa sana na akamuomba kuwa waziri mkuu( Chief secretary of state).Baada ya hapo vituko ndio vikaanza.Mwezi wa tatu (march),raisi Regan alishambuliwa kwa risasi katika jaribio la kumuua,risasi ilimpata kifuani na akakimbizwa hospitali kuu ya kijeshi kutibiwa.Chief of staff Haig akaona hapo ndio mahali pa kuonyesha vituko vyake.Haraka alitokea kwa waandishi wa habari na kuwaambia yafuatayo:"Constitutionally, gentlemen, you have the President, the Vice President and the Secretary of State in that order, and should the President decide he wants to transfer the helm to the Vice President, he will do so. He has not done that. As of now, I am in control here, in the White House, pending return of the Vice President and in close touch with him. If something came up, I would check with him, of course."
maana yake
" Waungwana ,kikatiba mlolongo wa madaraka ni raisi,makamu wa raisi halafu waziri mkuu (ambaye alikuwa yeye),na kama raisi akitaka kuhamisha madaraka kwa makamu wake wa raisi atafanya hivyo,lakini kwa sasa hajafanya hivyo.Mimi ndio mdhibiti hapa Ikulu.Namsubiri makamu wa rahisi arudi na nitamgusia naye kwa karibu na kama jambo likija, napenda kuangalia pamoja naye, bila shaka".
Wengi waliposikia maneno yake walishikwa na bumbuwazi,manake Marekani ni nchi imejengwa kufuata misingi ya kikatiba na yeye Haig hakuonyesha kuifahamu wala kuiheshimu katiba.Lakini yeye alitaka kuituliza nchi kwa kuonyesha ujasiri wake wa kijeshi kwa wananchi wa marekani ambao walishaanza kuchanganyikiwa kwa hofu kubwa baada ya raisi wao kupigwa risasi.Alitaka kuwapa uhakika kwamba kila kitu kiko sawa.
Kwakawaida katiba ya Marekani inasema raisi akishindwa kuongoza nchi kwa ugonjwa au akifa ghafla ili Vice president au secretary of state aongoze nchi inabidi spika wa bunge,na rais pro tempore wa Senate (wakati huo, J. Strom Thurmond), wajiuzulu na kuchukua wadhifa wa vice president .Na utaratibu huo huchukua muda.
Miaka mingi baadae mwaka 2001 aliulizwa kwenye kipindi cha 60 minutes alikuwa na maana gani akisema "i'm in control here", akajibu "I wasn't talking about transition. I was talking about the executive branch, who is running the government. That was the question asked. It was not, "Who is in line should the President die?"
No comments:
Post a Comment