Sikiliza Clouds FM Live station ya watu.

Wednesday, March 31, 2010

Jamani mtamu wangu( mysweetie) umepata barua kutoka kwa nani tena mbona waniogepesha?

Michelle alipata barua akitembea nje kwenye bustani yake ya ikulu kutoka kwa mtoto mdogo.Alikuwa anamuuliza kama anapenda ice cream na cake,na kwamba angefurahi kama angetembelea shule yake.Halafu alimwandikia kwamba msalimie na Barack.Michelle akaamua amuite Barack aisome mwenyewe.Huko Afrika kwetu yaani Raisi asome barua kutoka kwa mtoto au akae  kujibu maswali ya watoto ni kitu hakionekanagi mara nyingi.Nakumbuka shule niliyosoma muhimbili pimary yaani mwalimu mkuu akitokea tu inabidi ukimbie manake anaweza akakuwasha viboko vitatu au vinne kwa kuzulula hovyo.Labda tutafika siku moja kujua kwamba binadamu wote ni sawa,na wanahaki ya kusikilizwa bila kujali umri wala kabila.

No comments:

Post a Comment