Sikiliza Clouds FM Live station ya watu.

Wednesday, May 26, 2010

Amepotea tumsaidie mwenzetu ampate nduguye

Habari nilizozipata hivi punde ni kwamba Rafiki yangu mmoja hapa Ohio ninapoishi amempoteza ndugu yake huyo kama picha na maelezo ya polisi yanavyoonyesha.Ni habari za ukweli kabisa na zinazohuzunisha.Huyo dada alikuwa anaishi maeneo ya los angels.Najua familia yao iko na hofu kubwa sasa hivi kwa kumpoteza dada yao, kwa yeyote mwenye habari zake apige simu polisi los angeles au awaandikie barua pepe.Tumsaidieni mwenzetu apatikane jamani.Watanzania popote mlipo mnaombwa kushikia bango hilo hadi apatikane.

Saturday, May 15, 2010

Kicheko kwa siku hupunguza kumwona dakitari

Today, I handed my PhD dissertation, which I have spent the past year researching and writing full-time. Last night, my roommate set an autocorrect on Word that changed "neither" to "nigger." I didn't notice until after I handed it in. My professor is black. FML

Tuesday, May 11, 2010

Tanzania one Hasheem Thabeet

Wakwetu wenyewe (Tanzania one).Hasheem Thabeet akijitahidi kumzuia Lebron James.Kwavile ni Mtanzania wa kwanza kuchezea NBA tangu hiyo ligi ianzishwe miaka ya sitini inabidi apewe heshima yake,hata kama hafanyi vizuri sana kama ambavyo wengi tungemtarajia.Mungu aendelee kukubariki Hashim na uendelee na uwe na afya na mafanikio makubwa huko mbeleni.Watanzania wote tuko nyuma yako ukifanya vizuri au vibaya.Tunajua sio rahisi lakini kaza buti uendelee mbele.

Zilipendwa

Nakumbuka jamaa alipokuja bongo nilikuwa darasa la tatu mwaka 1990.Kwakweli nakumbuka msisimko wa watu mitaani,hakuna habari nyingine yoyote ilikuwa inaendelea.Na wakati huo kulikuwa hakuna cha ITV wala redio one kwahiyo kila kitu ni gazeti la uhuru au mfanyakazi,nilikuwa nashindwa kusoma daily news manake kiinglishi kilikuwa notirichebo.haha!



Jamaa chinja chinja Idi Amin dada akienda kumsalimia nyerere,sijui hapo nyerere anafikiria nini huku akimchekea,I wish waliokuwepo wangetupa stori .

Barua ya mzee kifimbo kwa mabepari

Mzee Nyerere aliwaandikia barua makabaila na kuwaambia sisi huku kwetu mashindano yenu ya nyuklia hayatuhusu,sijui nani ana nguvu kuliko nani,kama vile kwenu nyinyi ambavyo hamjali kuhusu sisi walalahoi kama tumekula au hatujala.Akaongeza nyie huko hamlali kwasababu ya kuhofia kulipuana wenyewe kwa wenyewe sisi huku hatulali kwasababu hatuna muhogo na nyama na hatujui tutaipata wapi.