Sikiliza Clouds FM Live station ya watu.

Sunday, July 24, 2011

UHURU KWA WATU WOTE NI THAMANI KUBWA SANA

Watu wetu kule Tanzania wanazungumza sana juu ya ukosefu wa bidhaa na uchaguzi finyu.Ukosefu wa umeme na maji safi ingawa wana hela za kulipia na wanamahitaji makubwa sana,ukosefu wa hospitali zenye tiba nzuri na za kutosha kusaidia wananchi wote,sheria mbovu zilizozorota kuanzia sheria za barabarani mpaka za uendeshaji wa biashara na usalama.
    Nchi zilizoendelea serikali zao zinaboresha na kuangalia tu utendaji wa wananchi wake na makampuni ya kibiashara lakini haijihusishi  kwenye shuhuli zozote za kuchagulia au kuamua watu wafanye nini.Filosofia ya nchi zilizoendelea kiviwanda ni kwamba kama tunania ya kufanya maisha ya watu wetu kuwa mazuri sana,jinsi ya kufanikisha hilo ni kuwapa kila mwananchi uhuru wake wote.Sababu ni kwamba Uhuru wenyewe kwanza kabisa ni kitu kizuri kwa binaadamu wote na pia kama kila mtu yuko huru basi ataweza kujiamulia mambo yake mwenyewe na kuchagua mambo yanayompendeza yeye mwenyewe kwa manufaa yake bila kuamuliwa na mtu yeyote.Jinsi ya kuuzidisha uhuru wa kila mtu mpaka kileleni kabisa ni kuwaongezea uchaguzi wa kila kitu chenye thamani kwenye maisha yao.Wanapokuwa na mambo mengi ya kuchagua wanakuwa na uhuru zaidi na wanapokuwa na uhuru zaidi maisha yao yanakuwa mazuri zaidi.

   Mfano mzuri nikienda dukani kununua dawa ya mswaki kuna aina 52 ambazo zote zinatangaza kwamba zinafanya kazi nzuri ya kusafisha na kung'arisha meno.Kampuni yangu ya bima ya afya wamenipa mhimili wa madaktari wa kuchagua kama dakitari wetu wa familia,mpaka sasa wako 24 bado sijachagua hata mmoja manake nimeongea na kila mmoja anasema anatoa huduma nzuri,natafuta shule za chekechea kwa mtoto wangu Makayla nae anapata shida kuchagua pia kwahiyo anabaki kusema anataka kwenda shule rafiki zake wanayoenda, bima yangu ya sheria (legal insurance) nao wamenipa mhimili wa wanasheria wa kuchagua kama nikipata tatizo la sheria bado nimeshindwa kuchagua mwanasheria,nilipokuwa nataka kununua gari nilikuwa nashindwa kuchagua,je ni honda,toyota,chevy,ford,gmc,mitsubishi na listi inaendelea zaidi na zaidi.Na kwenyewe ndani ya honda au toyota kuna aina nyingi pia.Kila aina ina manufaa na matatizo yake.Uchaguzi wa bidhaa fulani kwasababu ya manufaa kadhaa kunasababisha kukosa manufaa ya bidhaa ambazo hazimo kwenye chaguo.Wasomi wa kiuchumi wanaita ukosefu huo gharama mbadala (opportunity cost).Hii ndio shida mojawapo ya watu wanaoishi kwenye nchi zilizoendelea kiviwanda.
Kwa hivyobasi ilituweza kusonga mbele kwa pamoja ni muhimu kila mtu kuutambua uhuru wake.
Asanteni sana,
Wasalaamu David.

No comments:

Post a Comment